Duration 3:35

MKUU WA WILAYA UVINZA KIGOMA, AAGIZA MADARASA KUJENGWA USIKU KWA USIKU, WANAFUNZI WASIKAE CHINI.

689 watched
0
5
Published 29 Nov 2021

UVINZA - KIGOMA. MADIWANI na Wananchi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, wameuomba uongozi wa Wilaya Hiyo Kuongeza Kasi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa, Kwa Lengo la Kuondoa Usumbufu wa kusoma wakiwa wamekaa chini kwa kukosa miundombinu rafiki ya kujifunzia, Kwa Wanafunzi Wanaotalajiwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwakani. Wamesema kutokana na wingi wa wanafunzi waliofauru kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 juhudi na ushirikiano wa pamoja ni muhimu ili kufikia adhima ya Serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule Shikizi, Msingi na Sekondari wanapata elimu katika mazingira bora ya kujifunzia. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Uvinza Jackson Mateso amesema licha ya uwepo wa mazingira magumu ya kufikika kwa vijiji vilivyopo ukanda wa ziwa, wanaendelea na juhudi kuhakikisha wanafikia lengo la kukamilisha madarasa hayo kwa kushirikisha wananchi na viongozi wengine. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Uvinza Hannafi Msabaha ameeleza kuwa matarajio ni kuhakikisha ifikapo Desember 15 mwaka huu madarasa yote yanayojengwa yawe yamekamilika na kwamba italazimika ujenzi kufanyika hadi usiku kwa kutumia taa, kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo. Jumla ya Madarasa 118 kwa shule za Msingi na Sekondari na shule shikizi madarasa 78 yanatakiwa kukamilika desember 15 mwaka huu, yote yakijengwa kwa fedha za KOVID 19 zilizotolewa na serikali Kuu. MWISHO.

Category

Show more

Comments - 1