Duration 23:31

GIVE ME THAT MOUNTAIN - PASTOR SUNBELLA KYANDO

10 466 watched
0
159
Published 2 Dec 2021

Kalebu anamkumbusha Yoshua kuhusu ahadi na kiapo alichoapa Musa kwa Mungu kuwa atampa nchi baada ya kuingia Kanaani kwa ajili ya wema na utimilifu wake kwa za Mungu.Kabla ya kuingia Kanaani Musa alituma wapelelezi wakapeleleze kwenye hiyo nchi(Kanaani) na wapelelezi kumi walikuja na taarifa mbaya kasoro Yoshua na Kalebu peke yao,na kwa sababu hiyo Musa akamuapia Kalebu kwa Mungu kuwa watakapoingia Kanaani kuna nchi atampa. Musa hakufanikiwa kuingia Kanaani kwa sababu alimkosea Mungu na Mungu akamwambia kuwa hatoingia ile nchi.Wakati Kalebu anaahidiwa ahadi hii alikuwa na umri wa miaka 40 na ikapita miaka 45 zaidi bila yeye kupewa hiyo nchi. Wakati huo watu wa Yuda walikuwa wamemfuata Yoshua kwa sababu kuna maeneo walikuwa wakiyataka,Kalebu naye akaenda na akamkumbusha Yoshua juu ya ahadi aliyoahidiwa maana wakati Musa anaahidi Yoshua naye alikuwepo. Na Kalebu hakuishia hapo,alimwambia Yoshua eneo analolitaka,nchi iliyopo katika mlima Horebu.Ukisoma mstari wa 12 utaona kitu kikubwa sana;Kalebu anasema kuwa kama ambavyo alikuwa na nguvu alipopewa ahadi hii akiwa na miaka 40 vivyo hivyo bado ana nguvu za kupigana vita hata katika miaka hiyo 85 aliyonayo.Kwa maana nyingine ni kuwa, kutokana na ahadi ambayo ipo kwenye maisha yake mwili wake haukutakiwa kukua na kuishiwa nguvu maana atazihitaji kwenye kumiliki ahadi yake.Mungu ilibidi aende kinyume na kanuni za mwili kuwa hata katika miaka 85 aliyonayo bado ana nguvu za kupigana vita na jeshi na akashinda. Mungu anapokupa ahadi hata kama kanuni ya mwili hairuhusu bado Mungu yupo juu ya kanuni zote.Kama una ahadi ya kupata mtoto kwenye maisha yako,hata kama kanuni ya mwili inasema umri wako umeenda sana na huwezi tena kushika ujauzito lakini kwa Mungu hakuna kisichowezekana. Lakini pia Kalebu alijua kuwa kuwa na nguvu za mwili tu haitoshi kushinda vita,alihitaji pia Neno la Mungu kutoka kwa Yoshua.Neno la Mungu huwa limebeba nguvu lakini pia neema ya kukusaidia,kuwa na nguvu bila kuwa na Neno la Mungu bado hutoweza kushinda. #PastorSunbella#GiveMe#ThatMountain

Category

Show more

Comments - 26