Duration 2:30

HATIMAE KILIO CHA BANDARI KILWA CHA SIKIKA

179 watched
0
1
Published 6 Oct 2021

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais wa awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametenga shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari ya uvuvi wilayani Kilwa, Lindi. Mheshimiwa Majaliwa amesema mradi huo wa ujenzi wa bandari ya uvuvi utasaidia kuongeza kasi ya uvuvi wa kisasa na biashara ya samaki ili kuongeza pato la Taifa na kuboresha maisha ya wananchi wanaotegemea sekta hiyo. Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 6, 2021) wakati akizungumza na watumishi, madiwani na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika mkoa wa Lindi.

Category

Show more

Comments - 1