Viungo katika mitandao yetu ya jamii;
https://www.instagram.com/matrich_investing/?hl=enhttps://www.facebook.com/Matrich-Investing-104068614639938/https://twitter.com/MatrichInvesti1?s=09
MAELEZO KUHUSU UWIANO HUU
Haya ni mahesabu yanayochukuliwa baada ya kuchukua dhima jumla ya kampuni na kuigawanya kwa mtaji wa biashara.
Uwiano huu unatumika kuthamini uwezo wa kampuni hiyo katika kujiinua. Inatumika kama kipimo cha kuangalia kama kampuni inafadhili opresheni zake zaidi kwa kutumia madeni au mtaji wake wenyewe
Inatumika pia kutazama uwezo wa mtaji wa wanahisa katika kufunika madeni yake yote katika kipindi kigumu cha biashara
Katika uchunguzi wa kutafuta hisa nzuri ni vyema zaidi uwiano huu ukawa mdogo ukiashiria ya kwamba biashara inaendeshwa zaidi na mtaji wa wanahisa kuliko dhima jumla ya kampuni. Uwiano huu unapaswa kuwa chini ya 0.8 ili itambulike kama kiwango kizuri cha madeni kwa mtaji (isipokuwa mashirika ya kifedha kama benki)
MAHESABU YAKE
𝑫𝒉𝒊𝒎𝒂 𝒋𝒖𝒎𝒍𝒂/𝑴𝒕𝒂𝒋𝒊 𝒘𝒂 𝒘𝒂𝒏𝒂𝒉𝒊𝒔𝒂