Duration 6:39

MRADI WA NYERERE ULIPOFIKIA ,MRATIBU AELEZA HATUA MUHIMU ZA MRADI

17 418 watched
0
94
Published 20 Apr 2021

Mradi huu ambao awali ulijulikana kwa jina la Stiegler’s Gorge na sasa unaitwa Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) utazalisha umeme wa Megawati 2,115. Umeme huu unatarajiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa Tanzania; nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi katika Afrika Mashariki. Eneo la mradi liko Kusini Mashariki mwa Pori la Akiba la Selous; pori lenye ukubwa wa zaidi ya kilometa za mraba 50,000. Mradi unapakana na mikoa ya Pwani na Morogoro eneo litakalotumika kwa ajili ya mradi litachukua kilometa za mraba 914 tu huku kati ya hizo eneo la shughuli za ofisi, vituo vya kupozea na kusafirisha umeme likichukua kilometa za mraba 61.13 na zilizobaki sehemu kubwa itakuwa bwawa la maji. Aidha, taarifa zinaonyesha kuwa vyanzo vya maji vya Mto Rufiji ambavyo ndio chanzo kikuu cha mradi huo ni Mto Kilombero; ambao unachangia maji kiasi cha asilimia 65, Mto wa Ruaha Mkuu unachangia asilimia 15 na Mto Luwegu unachangia asilimia 19 ya maji yote. Asilimia moja iliyobaki inmachangiwa na vyanzo vingine vidogo vidogo.

Category

Show more

Comments - 8